What are People Saying About NGUZO

Ernest

Ernest Mwanri – Toronto, Ontario

“Kama lilivyo jina la umoja huu, sote tuliovutwa kujiunga ni ili kutatua shida ambayo ipo wazi kwa wengi. Tupo mbali na nyumbani penye familia tuliozaliwa nazo.

Sote twajua msiba ukitokea mchango sio kuchimba kaburi, bali ni kutafuta hela za kulipia gharama nyingi na kubwa za mazishi kwa nchi hii tuliochangua. Iwe ni kuzika hapa, au kusafirisha kwenda Tanzania, hitaji ni lilele la pesa.

Na unapoondoka mhimili na mlezi wa familia madhara huwa makubwa. Nakumbuka alipofariki Millicent ambaye ingawa alikuwa Mkenya, Watanzania wengi tulimjua kwani alishiriki nasi katika matukio mengi. Hali waliobaki nayo watoto ilikuwa ngumu.

NGUZO yetu hii itasaidia sana kuwepo kwa msaada wa haraka kwa wanafamilia wanaobaki haswa wakati tukio ndio tu limetokea na mshituko ni mkubwa.

Shukurani nyingi kwa waliobuni na kuandaa umoja huu – NGUZO Daima!

Dina Mrango

Dina Mrango – Toronto, Ontario

“Mimi nimeishi hapa miaka mingi nimeona jinsi tunavyohangaika mara mmoja wetu anapofariki. Nimekuwa nasubiri umoja wa kusaidiana kama huu. Kwa kweli NGUZO itatusaidia sana kusaidiana kwa haraka na utulivu zaidi pindi msiba utokeapo

Kuna faida kadhaa za kujiandaa na gharama za mazishi, mfano:-

  • Familia inakuwa na amani kitokeapo kifo kwani wanajuwa wataweza gharamia mazishi kirahisi
  • Familia inapata muda wa kuomboleza bila kusumbuka na kutafuta fedha za kugharamia mazishi kupitia harambee kwenye jumuiya
  • Kuwa na uwezo wa kugharamia mazishi kunafanya maamuzi ya maziko kuwa ya amani na muda mfupi zaidi.

Kwa mimi na familia yangu kujiunga na NGUZO kumeongeza amani hiyo.”

Sania Esmail

Sania Esmail – Barrie, Ontario

“Mara nyingi misiba ikitokea kwa uzoefu wangu, kumekuwa na changamoto kukusanya michango kwa njia ya simu au barua pepe. Vilevile msiba utokeapo ghafla, wengi wetu tunakuwa hatujajiandaa.

Kama tunavyofahamu misiba haitabiriki, hivyo si rahisi kujipanga kwa kuwa siku hazifanani. Leo naweza kuwa na $30 na kesho nina $20. Kwa hiyo mchango nitakaotoa utakuwa wa kulingana na uwezo niliokuwa nao kipindi hicho.

Nguzo imeturahisishia kazi na kuweka usawa kwa wanajumuia wote. Najua kabisa kiwango nitakachotoa kitakuwa sawa kwa watu wote watakaofikwa na msiba.

Napenda kutoa pongezi nyingi kwa wanajumuia wenzetu waliotumia muda wao kuandaa na kuendelea kuuboresha huu umoja kwa ajili yetu sote.”

Video Testimonies